UNCTAD inaweza kuweka msingi muafaka wa maendeleo baada ya matatizo:Migiro
Naibu KM Asha-Rose Migiro |
Katika ujumbe huo uliowasilishwa kwa niaba yake na naibu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro unasema kongongamano hilo umefanyika wakati muafaka kujadili mikakati muhimu ya kukabiliana na hali ya sasa ya utandawazi.
Bi Migiro ameongeza kwamba matatizo makubwa ya kiuchumi yaliyoikumba dunia hivi sasa tangu miaka ya 1930 yanamliza miaka kadhaa ya ukuaji wa uchumi na yanadhihirisha wazi hatari iliyopo katika masoko ya fedha duniani.
Wakati mdororo ulianzia katika nchi nyingi zilizoendelea kiuchumi atharin zake zimeikumba dunia nzima na zinaendelea kuathri matarajio ya maendeleo ya nchi nyingi masikini.Tangu wakati huo ufufuaji uchumi umekuwa ukilegalega na kuendelea kuyumba katika nchi nyingi"
Bi Migiro ameongeza kuwa kongamano la 13 la UNCTAD lazima liangalie sababu za matatizo na kubaini hatua za kuzuia yasitokee tena.
0 comments :
Post a Comment