Hot News
Loading...

UJUMBE WA WIKI YA MAELEWANO YA KIDINI DUNIANI


Dar es Salaam - Kwa mabilioni ya watu duniani  kote, imani ni msingi muhimu wa maisha. Imani inampa mtu nguvu wakati wa shida na kujisikia kama mwanajamii. Watu wengi wanaishi kwa maelewano na majirani zao bila kujali imani zao, lakini kila dini pia ina watu wachache ambao wako tayari kuwalazimisha watu wengine kufuata mafundisho ya imani fulani kwa kutumia nguvu bila kujali haki za watu hawa kiimani. 
Matendo haya ni dharau kwa urithi na mafundisho ya dini zote kubwa. Pia yanakwenda kinyume na Tamko  la Haki za Binadamu ambalo linasisitiza haki ya uhuru wa mawazo, dhamiri na dini. Ni muhimu  kuwawezesha wale wenye imani ya wastani kusimama thabiti dhidi ya nguvu za uhafidhina wa kidini. Hili linaweza tu kufanikiwa kama kuna uongozi thabiti.
Mwezi ujao mjini katika mkutano wao mjini Vienna, Muungano wa Ustaarabu (Alliance of Civilizations), utaendelea na juhudi za kuunganisha imani na tamaduni. Ikiwa ni kwa kiwango cha ulimwengu mzima au kijamii, viongozi wa kidini na kiutamaduni wanao wajibu wa kuzungumza lugha inayotoa ujumbe wa kuvumiliana na kuheshimiana. Huu ndiyo ujumbe mkuu wa Wiki ya Maelewano wa Kidini Duniani.
Ni lazima tuende kwa vijana na ujumbe wa matumaini. Mara nyingi kutokana na  kutengwa, kukosa ajira, na kukosa mustakabali wa uhakika, vijana wanajikuta katika mazingira ambayo wanavutwa kirahisi na wale wenye imani kali za kidini. Tunahitaji kufichua ubatili wa vivutio hivi na kuwapa vijana mazingira mbadala.
Haya hayawezi kufanikiwa kwa maneno tu. Vijana wanahitaji ajira na kuwa na hisa ya kueleweka kwenye mustakabali wanaoweza kuuamini. Umoja wa Mataifa kwa sasa uko katika mchakato wa kutengeneza ajenda ya maendeleo endelevu –baada ya 2015. Lengo letu ni kuondoa umaskini uliokithiri katika kipindi cha uhai wetu na kukuza uchumi unaotoa fursa sawa kwa wote bila kuharibu mazingira. Kufanya hilo, tunahitaji ushiriki wa wahusika wote—wakiwemo vijana na jumuia za kidini.
Tunaishi katika nyakati za mageuzi—kiuchumi, kimazingira, kidemografia na kisiasa. Mapito haya yanaleta matumaini na pia hali ya wasiwasi. Kazi yetu ni kuhakikisha kwamba matumaini yanashinda, na kazi yetu itakuwa rahisi iwapo wafuasi wa imani zote watashirikiana kufikia lengo moja. Tusisahau kwamba kinachotugawa sisi ni kidogo sana ukilinganisha na kile kinachotuunganisha. Tukifanya kazi kwa pamoja, tunaweza kufikia malego yetu ya ustawi katika amani, mafanikio, mwili na imani. SOURCE
Share on Google Plus

About un chapter amucta

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

Redio ya Umoja wa Mataifa

UNIC Dar es Salaam