Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki muhimu kwa watu, na ni uhuru unaozidi uhuru wa aina yoyote ile na kutoa msingi wa utu wa mtu. Haya yameelezwa katika taarifa ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova. Taarifa yao ikitoa ujumbe maalumu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari imesema, vyombo vya habari huru, vinavyojumuisha wote na vinavyojitegemea ni muhimu katika kufanikisha azima hii.
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua kuhusu usalama wa waandishi wa habari na masuala ya ukatili, wakiongozwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na bodi ya wakurugenzi wa Umoja wa Mataifa wameidhinisha hapo April 13 mwaka huu njia za ushirikiano katika mfumo wa umoja wa mataifa ambazo zitalinda usalama wa waandishi wa habari.
(MAHOJIANO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI)
0 comments :
Post a Comment