SOTE KWA ROHO NA MIOYO YA PAMOJA HUISHI NA KUTAMBUA MAISHA NA THAMANI YAKE PALE TUWAPO WAZIMA LAKINI NI UKWELI USIOPINGIKA TUMEKUA NA KAWAIDA YA KUSAHAU KIDOGO THAMANI HII. LABDA NDIPO NAWEZA SEMA KUA MUNGU AMETUPA NAFSI HII PEKEE YA KUWA NA UTASHI BINAFSI NA HUTUKUMBUSHA UMUHIMU HUO WA TUNU YA MAISHA KWA MATUKIO MENGI AMBAYO KWA HALI YA KIBINADAMU NI VIGUMU KUVIZUIA VISITOKEE NA VIKITOKEA NI VIGUMU KUONESHA HISIA ZA MGUSO. KIUKWELI VITU AU MAMBO MOJAWAPO AMBAYO KWA BINADAMU HUWA NI MAGUMU NA HUOGOPWA NA WENGI NA KUSHITUSHWA NAYO MARA YAKITOKEA BAADHI YAKE HUWA NI VIFO NA HIVYO MIOYO HUAMKA NA KUTOA MAJUTO MENGI JUU YA MAUMIVU YA KILIO HUSIKA, IMETUWIA VIGUMU KUPOKEA, KUAMINI, KUKUBALI NAHATA KUTOPENDA KUENDELEA KUSIKIA TAARIFA AMBAZO MASIKIO YANASIKIA NA PENGINE MACHO KUONA NA KUFANYA HITIMISHO BINAFSI KWA KUKUBALI YANAYOTUSIBU. NI MMOJA WA WANACHUO MWENZETU, MPENDWA MWENZETU TULIEMPENDA NA HASA KUSHIRIKIANA KATIKA SHUGHULI ZA KITAALUMA KWAMBA YU MIKONONI MWA HAKI ZA MWENYEZI MUNGU. MUNGU IWEKE MAHALI PEMA ROHO YA KAPANI JANUARY KATIKIA WITO NA KUTIMIZA HARUSI YAKE YA MWISHO YA MAISHA. PUMZIKA KWA AMANI
UN CHAPTER INAWAPA POLE WALE WOTE WALIOFIKWA NA KUGUSWA NA MSIBA HUU.
0 comments :
Post a Comment